in ,

Umoja wa Ulaya wamuita balozi wa Urusi

Umoja wa Ulaya umemuita balozi wa Urusi Vladmir Chizhov, baada ya nchi hiyo kuwazuia wanasiasa wanane wa Ulaya kuingia Urusi. Msemaji wa masuala ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Peter Stano amesema watafikisha ujumbe wa kulaani na kuukataa uamuzi huo. 

Stano amesema Balozi Chizhov atapokelewa na maafisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Ulaya katika mkutano unaotarajiwa kufanyika baadae leo. 

iki iliyopita, Urusi iliwapiga marufuku wanasiasa wa Umoja wa Ulaya kuingia nchini humo katika kujibu vikwazo ilivyowekewa na umoja huo, ambavyo imesema sio halali. Miongoni mwa maafisa hao ni Spika wa Bunge la Ulaya, David Sassali na Makamu Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya, Vera Jourova. Umoja wa Ulaya na Marekani zimechukua hatua kadhaa dhidi ya Urusi, kuanzia kuwafukuza wanadiplomasia na marufuku ya kuingia kwenye nchi hizo hadi vikwazo vya kiuchumi.

Waziri Mkumbo atinga TBS “hakuna sababu ya msingi kupandisha bei ya mafuta”

WHO: Small Ebola Outbreak Contained in DR Congo | Muhabarishaji News Agency