AfricaSwahili News

UN yataka usalama kuimarishwa DRC baada ya watu 19 kuuawa

Watu 19 wameuawa katika msururu wa mauaji nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Madaktari wasiokua na mipaka au Médecins Sans Frontières wamesema raia 10 waliuawa baada ya hospitali kushambuliwa katika mji wa Boga mashariki mwa DRC siku ya Jumatatu.

Miili kadha iliripotiwa kupatikana baada ya wakulima kushambuliwa katika mpaka kati ya mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri.

Mashambulio ya mara kwa mara yamekuwa yakifanywa katika eneo hilo na Vikosi vya Allied Democratic au ADF– moja ya makumi ya makundi yaliyojihami mashariki mwa DRC.

Matthias Gillman, msemaji wa kikosi cha walinda usalama wa wa Umoja wa Mataifa – au Monusco – ametoa wito wa kupelekwa kwa maafisa zaidi wa polisi katika eneo hilo:

“Eneo hili limekuwa hatari kwa muda mrefu kwa sababu liko vijijini, ni vigumu kufika, ni kubwa na halina maafisa wa usalama wa serikali wanaohitajika, ndio sababu vikosi vya Monusco … vinataka serikali kuimarisha uwepo wake.

 

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Related Articles

Back to top button