Mara nyingi hali ya kichefuchefu kwa wajawazito imekuwa ni kawaida kwa wajawazito wengi. Hivyo watalam mbalimbali wa masula ya afya wanasema ili kuondokana na tatizo la kichefuchefu kwa wajawazito wanashauriwa kufanya yafutayi;
1. Tumia limao au ndimu
Limao au ndimu vina uchachu ambao husaidia kukata hali ya kichefuchefu. Kata limao na nusa, harufu ya limao itasaidia kupunguza hii hali ya kutapika. Pia unaweza ukakamulia limao kwenye chai au maji ukanywa. Unaweza pia kunusa maganda au majani ya limao maana husaidia pia kupunguza hali ya kichefuchefu.
2. Kula vyakula venye protini na vitamin B6
Vyakula venye protini kwa wingi na vile vyenye vitamin B6 humfanya mama apunguze hali ya kichefuchefu. Inashauriwa mama mjamzito aepuke kula vyakula venye viungo vingi, mafuta au vilivyokaangwa kwa muda mrefu sana. Vyakula hivi huweza kuzidisha hali ya kichefuchefu na kutapika balada ya kuiondoa.
3. Tangawizi
Tangawizi hupunguza hali ya kichefuchefu, hivyo unaweza kuitumia kwenye chai au unaweza kukata kipande kidogo cha tangawizi na kutafuna kidogo kidogo.


Hivyo ni baadhi ya vitu kati ya vingi vinavyoweza kupunguza kichefuchefu.

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles