More
  - Advertisement -

  Waandishi wa habari Manyara wafanya jambo wakisherekea Uhuru wa vyombo vya habari

  -

  - Ad Keep reading below -

  Na John Walter- Manyara

  Klabu ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Manyara (MPC)  imeadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani kwa kutoa msaada wa vyakula kwa kituo cha watoto cha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu (MAHOCE) na kituo cha wazee cha Sarame Kata ya Magugu Wilayani Babati.

  - Ad Keep reading below -

  Mwenyekiti wa Klabu Zacharia Mtigandi amesema wametoa msaada huo ili kushiriki pamoja madhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari na watoto na wazee hao ili kuwapa faraja.

  Ntigandi amesema MPC iliamua kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani kwa kushiriki na watoto na wazee hao ikiwa ni mchango wao katika kusaidia makundi hayo yenye uhitaji.

  - Ad Keep reading below -

  Waandishi hao  katika kituo cha Manyara Holistic Centre (MAHOCE) mjini Babati wametoa mchele kilo 100 pamoja na mafuta ya kupikia lita 20.

  ALSO READ  VIDEO: Zitto aamua maamuzi mazito ''hujuma hii haivumiliki''

  Aidha kwenye kituo cha wazee Sarame waliwapatia mchele kilo 50, lita 20 za mafuta na viburudisho.

  Mkurugenzi wa MAHOCE Joshua Johnson amewashukuru waandishi hao wa habari kwa kuwatembelea na kuwapa msaada huo wa vyakula kwenye madhimisho hayo ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari.

  ALSO READ  Siri sita za kuanzisha biashara yenye mafanikio

  Amesema wanawahudumia takribani watoto 80 katika kituo hicho kilichoanzishwa mnamo  mwaka 2007 na kina watoto 80.

  - Ad Keep reading below -

  Pamoja na hayo klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Manyara, wamezindua   Blog ya chama ambayo itatoa fursa kwa waandishi kuutangaza mkoa kupitia taarifa zao watakazokuwa wanazichapisha na kuingiza kipato kupitia matangazo mbalimbali.

  Makamu Mwenyekiti wa MPC, Mary Margwe amesema kwa kipindi hiki wameadhimisha tofauti na miaka iliyopita ambapo walikuwa wanakutana na wadau mbalimbali wa habari wa mkoa huo.

  - read any article below now-
  Publisher
  Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

  Latest news

  Shocking Leicester display raises serious questions about ability to handle pressure

  Leicester's top-four hoodoo returned as they collapsed in the 4-2 loss to Newcastle United.

  Postpone LG election to avoid another legal gymnastics – ex-Oyo Gov, Alao-Akala tells Makinde

  A former Governor of Oyo State, Chief Christopher Adebayo Alao-Akala, has advised the incumbent Governor, Engineer Seyi Makinde, to without wasting more time, postpone...

  FBI hails EFCC for efforts on global crime war

  The Federal Bureau of Investigation (FBI) considers the Economic and Financial Crimes Commission (EFCC) a critical partner in the global fight against organized crime...
  - Advertisement -

  You might also likeRELATED
  Recommended to you

  - Advertisement -
  %d bloggers like this: