Advertisement Scroll To Keep Reading
AfricaSwahili News

Waandishi was Habari,Asasi za Kiraia wafundwa

Advertisement Scroll To Keep Reading

Na Thabit Madai, Zanzibar.

WAANDISHI wa Habari, Wana Asasi za Kiraia pamoja na Watendaji wa Serikali wametakiwa kuwa wabunifu na kutumia njia sahihi katika suala zima la utatuzi wa migogoro ndani ya Jamii.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Aidha wametakiwa kutengeneza Mashirikiano pamoja katika kufuatilia na kutatua migogoro inayoikabili jamii inayowazunguka.

Wito huo umetolewa na Afisa Ufuatiliaji na Tathimini wa Mradi wa Jenga Amani Yetu Khamis Haroun Hamad wakati akifungua mkutano wa Siku moja wa Majadiliano baina ya Watendaji wa Serikali,Asasi za Kiraia pamoja na Waandishi wa Habari ambapo Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar(ZLSC).

Afisa huyo amesema kuwa, Waandishi wa Habari,Wana Asasi za Kiraia pamoja na watendaji wa Serikali wana jukumu kubwa la utatuzi wa migogoro katika jamii inayowazunguka hivyo wanapaswa kuwa wabunifu na kutumia njia zilizosahihi ili wasiwe chanjo cha kuendeleza migogoro hiyo

Amesema, Jambo la msingi ni kuwa waangalifu wakati wa utatuzi wa migogoro sambamba na kuielewa vyema jamii ambayo wanafanyia kazi.

“Munapaswa kuwa na mashirikiano ya pamoja wakati wa ufanyaji kazi wenu lakini pia jambo la msingi ni kuwa waangalifu wakati wa utatuzi ili kila upande uweze kufaidika,” alieleza.

Hata hivyo alieleza kwamba, katika utendaji kazi wao wa kila siku wanapaswa kuzingatia namna ya kulinda Amani ya Nchi 

Aidha aliwataka washiriki wa Mkutano huo wa majadiliano kujenga Munganiko mzuri utakao saidia kuraisisha utendaji wa kazi wa majukumu yao ya kila siku.

“Hata hivyo munatakiwa kujenga mashirikiano baina yetu sambamba na jamii ili iwe na urahisi wakati wa utekelezaji wa majukumu yenu ya kila siku,”alisema.

Nae Mratibu wa Mradi wa Jenga Amani yetu Zanzibar,Jamila Maoud aliwataka washiriki wa Mkutano huo aliwaasa kuwa na weledi, busara na hekta wakati wa utatuzi wa migogoro inayoikabili jamii nzima.

“Unapotumia weledi,hekma na busara wakati wa utatuzi wa migogoro huwa ni nyenzo kubwa inayosaidia kwa kiasi kikubwa kutatua migogoro kwa njia ya Amani,”alieleza.

Hata hivyo akielezea Mradi wa Jnega Amani yetu alisema kuwa mradi ni wa miaka mbili ambao unatekelezwa     Zanzibar na Tanzania bara katika mikoa tofauti tofauti.

Alisema mradi huo unatekelezwa na shirika la search for Common Ground pamoja na kituo cha huduma za sheria Zanzibar ambapo wafadhili wakuu wa mradi huo ni umoja wa ulaya.

Mapema akiwasilisha Majadiliano ya pamoja ya Makundi  Mwandishi wa Habari kutoka Redio Zanzibar Takdir Ali alisema kwamba, migogoro mingi inayoikabili jamii ya Zanzibar ni pamoja na Migogoro ya Ardhi pamoja na Migogoro ya ndoa.

“Migogogro hii huwa ina sababu mbalimbali ikiwemo watu kukosa Elimu ya ndoa pamoja na kukosa elimu ya kina juu ya umiliki wa ardhi,”alisema.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.