By Sharon Sauwa

Dodoma. Serikali na mashirika ya kimataifa yanayotoa misaada na kufadhili miradi nchini wamefanya mkutano wa kupitia mpango wa pili wa ushirikiano wa Maendeleo wa mashirika ya Umoja wa Mataifa (UNDAP 11) unaomalizika Juni mwakani.

Kikao hicho watajadili na kupitisha mpango mpya wa miaka mitano wa UNDAP utakaoanza mwaka 21/22 na kumalizika 2027.

Akizungumzia kuhusu mkutano huo, leo Alhamisi Oktoba 7 2021, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Tutuba amesema kikao hicho kimeshirikisha viongozi kutoka sekta zinazopata misaada kutoka mashirika hayo na uongozi wa mashirika hayo.

Amesema mpango huo unajikita katika kuwezesha utekelezaji wa shughuli za maendeleo za afya, ustawi wa jamii, uhimilivu wa changamoto za maendeleo, ukuaji wa kiuchumi, utawala bora, haki za binadamu na jinsia.

Naye Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) Zlatan Milisic amesema mpango mpya wa ushirikiano katika ya Tanzania na mashirika hao utaonyesha tofauti ya utekelezaji wa shughuli nchini.

Amesema lengo ni kuhamasisha ushirikiano wa utekelezaji wa shughuli za maendeleo na kuwaleta pamoja wadau wengi katika katika kasi ya kufikia maendeleo endelevu (SDGs).

Advertisement

This article Belongs to

News Source link

About the Author

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

View All Articles