By Mwandishi Wetu

Dodoma. Wanachama 70 wamerudisha fomu za kuomba kuteuliwa kukiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Tanzania.

Akito taarifa baada ya kufungwa mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu leo Jumamosi Januari 15, 2022 Msaidizi Mkuu Idara ya Oganaizesheni CCM Taifa, Solomon Itunda amesema wanachama 71 walichukua fomu na waliorejesha ni 70 huku mmoja akishindwa kurejesha mpaka muda uliowekwa kuisha.

SOMA: Waliochukua fomu za uspika CCM wafikia 66

Amesema idadi hiyo ni baada ya wanachama watano waliojitokeza leo Jumamosi ambapo waliochukua fomu katika ofisi za chama hicho Dar es Salaam wakiwa wane huku mmoja akichukua Dodoma” amesema Itunda

SOMA ZAIDI:Wanachama 49 wachukua fomu kuutaka uspika

“Leo ni siku yetu ya mwisho ya kutoa na kupokea fomu za wanachama wetu walioomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Spika, jumla tuna wanachama 71 mpaka tunahitimisha leo” amesema nakuongeza

Advertisement

SOMA: Makada 30 wanaotaka kumrithi Ndugai hawa hapa….

“Katika wanachama hao wanaume wako 60 lakini wanawake wapo 11” amesema Itunda

Amewataja waliowaliojitokeza kuchukua fomu leo Dodoma ni Samweli Magero Magero huku Dar es Salaam wakijitokeza wanachama wanne ambao ni Rahim Rashid Ismail, Alex Mwita, Semistocles Rwegasira pamoja na Gragrey Nyalohala

SOMA: Tisa wachukua fomu CCM kugombea uspika

Uchukuaji na urejeshaji fomu hizo ulianza Jumatatu 10, 2022 na kuhitimishwa leo Jumamosi na baada ya hapo hatua zingine zitafuata za kumpata mwanachama mmoja wa kukiwakilisha chama hicho.

Akitangaza ratiba ya chama hicho ya kumpata mgombea wa nafasi hiyo Jumapili Januari 9 katika ofisi Kuu za CCM Kisiwandui Zanzibar, Katibu Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka alisema mchakato huo utahitimishwa Januari 31.

SOMA ZAIDI: CCM yatangaza ratiba uchukuaji fomu kugombea nafasi ya Spika

Shaka alisema Januari 17 sekretarieti ya halmashauri kuu ya Taifa itakutana kwa ajili ya kujadili wagombea na kuishauri kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa juu ya wagombea waliojitokeza.

Januari 18 hadi 19 kutakuwa na kazi ya kuchuja na kufanya uteuzi wa mwisho ambapo kamati kuu ya halmashauri kuu itafanya kazi hiyo.

Alisema kuanzia Januari 21 hadi 30 wabunge wa CCM watapiga kura kumpata mtu atakayekwenda kusimama bungeni kwa ajili ya kuomba kuchaguliwa kuwa Spika wa Tanzania.

This article Belongs to

News Source link

About the Author

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

View All Articles