in ,

Wanafunzi wa kidato cha 6 watakiwa kuacha udanganyifu

Na Thabit Madai,Zanzibar.

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar  Simai Mohammed Said amewataka Wanafunzi wa kidato cha sita kuachana na vitendo vya  udanganyifu  katika kipindi chote cha mitihani yao ya  Taifa ili kuweza kufaulu vizuri.

Amesema hayo wakati alipofanya ziara na kuwatakia mitihani mema Wanafunzi wote wanaofanya mitihani yao katika Skuli ya Aboud Jumbe Mwinyi ya Fuoni  Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, amesema suala la kupata ufaulu mzuri kunahitaji bidii katika masomo na sio kufanya udanganyifu wowote.

Simai amewasisitiza Wanafunzi kuondosha hofu wakati wanapofanya mitihani yao na badala yake wajiamini ili waweze kuleta matokeo mazuri na kuongeza viwango vya ufaulu kwa Taifa lao.

Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia wizara ya Elimu , wapo karibu na Wanafunzi hao ili kuhakikisha wanapata matumaini ya kufanya vizuri kwenye masomo yao.

Aidha  Simai ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha wanakua karibu na watoto wao ili kuwapa matumaini ya kufanya vizuri katika mitihani yao.

Pia Said amesema jumla ya Wanafunzi 2749 kwa Zanzibar wanafanya mitihani yao ya Taifa ya kidato cha sita ambapo wanawake ni  1428 sawa na asilimia 51.94 na wanaume  ni 1321 sawa na asilimia 48.05.

Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya Elimu Sekondari Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar  Asya Iddi Issa akizungumzia somo maalum la Sanaa(fine art), amesema Idara yake inajivunia kuwa na darasa la pekee la kidato cha sita la somo hilo  kwa Tanzania nzima na limeanza.kufanyiwa mitihani mwaka huu, ambalo linafundishwa katika Skuli ya Aboud Jumbe Mwinyi ya Fuoni.

Amesema darasa hilo hukuza  kirahisi  sanaa ambapo  ameiomba jamii kwa yeyote mwenye uwezo wa kuwawezesha sana hiyo kwa kushirikiana na wlWanafunzi hao  kuhakikisha wanawashirikisha katika matukio mbalimbali ili waweze kuonyesha vipaji vyao.

Jumla ya vituo 38 vitatumika kufanya mitihani ikiwa  Pemba ni vituo 10 na vituo 28 kwa Unguja kwa skuli za Serikali na binafsi.

 

Iran Navy capable of monitoring 2.70 bn km of open waters

NASS will not pass any law against press freedom – Lawan