Na Maridhia Ngemela, Mwanza

Shule ya sekondari Buhongwa inahitaji uzio wenye thamani ya zaidi ya milioni 100 kwa ajili ya ulinzi wa wanafunzi hususani watoto wa kike na wenye mahitaji maalum.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa bodi ya bonde la maji Mkoa wa pwani rufiji Florence Mahay aliyekuwa mgeni rasmi katika sherehe ya mahafari ya kidato cha nne yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Buhongwa Wilayani ya Nyamagana Mkoani Mwanza.

Mahay alisema ni haki ya kumpatia mtoto elimu hata kama anaulemavu wazazi waache tabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu nawao wanahaki zao za msingi kama watoto wengine hivyo ni vema tuzingatie kuwapatia elimu ili ije iwasaidie hapo baadae.

“Hii ni shule ya kipekee inawanafunzi wengi wa kike kuliko wa kiume na tumeona watoto wenye mahitaji maaluma wamefanya vizuri kuliko hata wasiokuwa na ulemavu wowote mfano huyu binti aliyepata Alama za juu yaani amepata point 7 ambapo ni daraja la kwanza katika mitihani yake ya Taifa ya kidato cha pili kuingia kidato cha tatu anaulemavu wa kutosikia lakini ameongeza kwahiyo wazazi embu tubadirike tuwasomeshe watoto kwa kuwaweka malengo ya baadae hata kama anaulemavu tuache kuwaficha huko hizi imani potofu tuziache alisema Mahay.

Florence aliongoza zoezi la harambee kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa shule hiyo ilikuweka usalama zaidi kwa watoto hao kwani wengi wao ni wasichana na wenye mahitaji maalum ambao wanaitaji uangalizi wa karibu na ulinzi ukiwa ni kipaumbele zaidi.

Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Christine Mchelle alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mahafari hayo alisema kuwa wadau wa elimu wajitokeze kwa wingi ili waweze kuchangia ujenzi huo kwani  lengo la kujenga uzio wa shule hiyo ambapo zaidi ya sh milioni 100 zinahitajika ilikuweza kumaliza tatizo hilo.

“Na shule yetu hii unawatoto wenye uhitaji maalum126 Kati ya hao 3 wakiume lakini wamegawanyika katika makundi mbalimbali walemavu wa ngozi wako 26,viungo 47,viziwi 39 ,wasioona 8 na uoni hafifu sita na wanafanya vizuri na hapa ufaulu wetu ni mzuri Sana ndiyo maana tunawanafunzi wengi kwani  mwaka huu tunawahitimu 510 wa kidato cha nne.

“Shule yetu ina jumla ya wanafunzi 2415 hakuna mzazi ambaye anayetamani kumpelekea mtoto wake shule ambayo haifanyi vizuri kwa hiyo bado nawasisitiza wadau wa elimu na wananchi wajitokeze kwa wingi  ujenzi huo  kutuchangia  vifaa mbalimbali ikiwamo  mifuko ya saruji, nondo,matofali na mchanga”,amesema Mchelle.

Naye diwani wa kata ya Buhongwa Joseph Kabadi alisema watoto wanajitahidi kufanya vizuri kwa hiyo leo hii tulikuwa na chagizo ili kuanza kujenga uzio kwa lengo la kuwaweka watoto wetu ulinzi.

” Mwaka jana tulijenga bweni kwa michango ya wananchi na Serikali wakamalizia jengo hilo kwa hiyo ninaamini  na uzio huu  watachangia  ili kuepusha changamoto ambazo zinaweza kujitokeza kwa watoto wetu.

“Mfano kuna vijana ambao walishawahi kuja hapa wakakata nyaya ambazo tumeziweka kama uzio  kwa ajili ya ulinzi wakataka kufanya fujo ila wanafunzi waliwaona wakaanza kupiga kelele vijana hao wakakimbia kwa hiyo tukiweka uzio imara tutazuia vitu kama hivi”, amesema Kabadi.