Wanajeshi wapatao wanane wameuawa na wengine kadhaa hawajulikani waliko baada ya hapo jana kuvamiwa na wanamgambo wa kundi linalojiita Dola la Kiislam – IS katika jimbo la Borno. 

Ni shambulio la pili la aina hiyo katika wiki mbili zilizopita kufanywa na tawi hilo la IS barani Afrika linalojiita ISWAP, ambalo limekuwa likifanya mashambulizi kwenye eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria kwa takriban miaka 12. 

Kundi la ISWAP limekuwa likijiimarisha katika eneo la Ziwa Chad tangu kamanda wa kundi hasimu la Boko Haram Abubakar Shekau alipouawa katika mapigano kati ya vikosi hivyo viwili vya jihadi mapema mwaka huu. Mzozo huo umesambaa hadi katika nchi jirani za Niger, Chad na Cameroon. 

Kutokana na hali hiyo, kumeundwa muungano wa kijeshi wa kikanda wa kupambana na vikundi vyenye misimamo mikali ya kidini ili kurejesha amani kwenye eneo hilo.

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles