Na Amiri Kilagalila,Njombe

Wananchi wa Lutala kijiji cha Mbongo wilayani Ludewa mkoani Njombe wanaomba kukopeshwa mashine ya kusaga na kukoboa nafaka ili kurahisisha kazi kubwa wanayoifanya kwa kusaga nafaka kutumia mawe na vinu ili kupata unga kwa ajili ya matumizi ya chakula na lishe kwa watoto.

Wito umetolewa na wananchi hao wakati wa ziara ya mbunge wa jimbo hilo wakili Joseph Kamonga alipofika na kueleza shughuli mbali mbali na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Ludewa.

John Edward (Mlope),Rosaria Haule na Angeus Mkinga ni miongoni mwa wananchi wa Lutala wamesema kwa miaka yote wamekuwa wakitumia vinu na mawe katika kusaga nafaka huku wengine wakisafiri umbali mrefu kupata huduma ya mashine.

“Siku zote tunatwanga mahindi kwa mkono kwenye vinu tunapata shida kwa kuwa hatua zake ni ngumu na ukitaka kufuata mashine basi lazime ubebe nafaka kichwani na kuenda maeneo mengine umbali wa masaa matatu”alisema Rosaria Haule

John Edward Alisema “Lutala tunakikundi kinaitwa tupendane chenye wanachama 34 tunaomba tukopeshwe mashine,sahizi tunaenda kusaga Iwela wengine wako Nsungu na wengine Mbongo hili tunaomba tusaidiwe sana”

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Joseph Kamonga,ameiomba ofisi ya maendeleo ya jamii kuwawezesha kikundi hicho kiweze kukidhi vigezo na kupatiwa mkopa ili kuwapunguzia changamoto ya kusafiri umbali mrefu.

“Niombe afisa maendeleo ya jamii hii mashine hapa ipatikane kwasababu watu wanasafiri kilomita nyingi sana kwenda kusaga ni bora tuwakopeshe ili waondokane nahii adha”alisema Kamonga

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles