Na Maridhia Ngemela,Mwanza

Wakaazi wa   kata ya kayenze  wamejitokeza kwa wingi  kuchimba msingi wa  kituo cha afya  kinachotarajia kujengwa kwenye mtaa wa   Nyabugali uliopo wilayani Ilemela Mkoani Mwanza.

 Hii ni baada ya serikali kupeleka  sh milioni 250 kwa ajili ya  kujenga kituo hicho ambacho kitapunguza  changamoto ya wananchi kufuata huduma za matibabu mbali.

Wananchi hao wamejitokeza kuunga jitihada za Serikali   kwa kuhakikisha  wanachimba msingi huo bila kusubili wakandarasi wowote kutokana na uhitaji wa kituo hicho ambacho kitapunguza changamoto ya kufuata matibabu mbali hususani kwa mama mjamzito.

Mbunge wa jimbo la Ilemela Dkt.Angelinemabula alipokuwa katika zoezi la uzinduzi wa ujenzi wa kituo hicho  kinachotarajia kuanza kijengwa  hivi karibuni amesema ni vema kila   mwananchi  kuwa mwaminifu ili kuweza  kupata kituo chenye ubora ambacho kitatoa huduma zote za matibabu.

” Tuendelee kumuunga mkono Rais kwa kusogeza karibu  huduma za matibabu  kwa wananchi ili kupunguza kero kwa jamii.

“Sisi kama wasaidizi wake na  niwawakilishi wa wananchi  tupo tayari kumuunga mkono ili kuhakikisha  kila jambo  ambalo amedhamilia kulifanya  tutalisimamia katika utekelezaji wa shughuli hizo na kutambua  matumizi ya pesa ili kupata kituo chenye ubora kinachokwenda na sera ya taifa.

Asemema mwaka 2019/2020  vituo viwili vya afya karume na Buzuruga viliboleshwa kwa sababu havikuwa na miundombinu kamili.

Amesema kituo hicho kikikamilika wilaya hiyo itakuwa na vituo vinne  huku kata 15 zitakuwa hazina  vituo hivyo lakini kwa jiografia ya mjini kituo kimoja kinaweza kuhudumia  kata mbili hadi tatu.

“Bado tunauhitaji wa kuwa na Tarafa zaidi ya moja ili kusogeza huduma kwa wananchi kwani tuna kata 19 kuwa na tarafa moja  bado ni changamoto lakini tunamshukru Rais kwa  maamuzi yake ya matumizi mazuri ya tozo ambazo zimeendelea kutozwa katika mazingumzo yake alisema kila tarafa itapata kituo cha afya na sisi  ni moja ya wanufaika wa  fedhahizo.
 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Ilemela Modest Aplinary amesema kituo hicho kitakuwa na jengo la wagonjwa wa nje,maabara na kichomea taka ni vema wananchi kujitoa kwa hali na mali ili kuendelea kuokoa fedha ambazo zingetumika kulipa watu kuchimba msingi huo hata hivyo ametoa matofali 10,000 kwenye ujenzi huo

 Mkuu wa Wilaya Hassan Masala amewapongeza wananchi kwa kuupokea mradi huo kwani atahakikisha fedha hizo hazikai kwenye akaunti na badala yake zinatafanya  kazi ambayo imekusudiwa   
ili kutatua changamoto kwa wananchi.

” Mtendaji msaidiane na kamati zilizoundwa  tunataka  kuona fedha hizi kuwanzia shilingi ya kwanza mpaka ya mwisho lazima zionekane kwenye karatasi imefanya jambo gani na kila iliyookolewa na wananchi kwa kujitolea itambulike imeokolewa kiasi gan lengo kupata zaidi ya haya majengo  tatu kwa ukamifu ili kumuonyesha Rais tulikuwa na shida.

“Serikali ipo pamoja na nyinyi na itaendelea kuwa karibu na ikiwezekana kabla ya miezi tunatamani  kituo hiki kiwe kimeanza kutoa huduma kwani fedha tunazo nguvu tunazo na nia tunayo na tumezionyesha hapa tunawashukru  wananchi wote kwa kuupokea mradi huu na kutoa eneo  sisi tutahalikisha fedha hazikai kwenye akaunti bali zinafanya kazi husika”,alisema Masala.

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles