in ,

Wananchi washirikishwe katika Miradi ya Maendeleo

Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) imesema kuwa ni muhimu sana Jamii kushirikishwa katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ikiwemo miradi ya ujenzi wa vituo vya afya na zahanati.

Kauli hiyo imebainishwa na Afisa  Maendeleo ya Jamii Bi. Hilda Mgomapayo ,kutoka  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wakati wa kikao kazi na Timu ya Uendeshaji  na Usimamizi wa Huduma ya Afya katika  Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli.

 Bi. Mgomapayo ameeleza kuwa ushirikishwji wa jamii unatoa fursa kwa Jamii kushiriki kwa kuchangia  nguvu kazi ikiwa Ni pamoja na kuchimba msingi, kukusanya mawe, kusomba mchanga na hata kuchangia fedha inapobidi.

“Hii hupunguza garama na ujenzi na hivyo kufanikisha mradi kukamilika na pia ina leta ‘ownership’ ya mradi  na kufanya usimamizi kikamilifu”, ameeleza Bi.Mgomapayo.

 Aidha ametoa wito kwa watoa huduma za afya kushirikiana na maafisa mafisa maendeleo ya Jamii ili  kuhakikisha wanafanya Uhamasishaji wa wananchi kujiunga na bima ya afya ya Jamii iliyoboreshwa (ICHF). 

Bi. Mgomapayo ameongeza kuwa HALMASHAURI ya Bumbuli iko chini Sana katika usajili wa wanachama wa ICHF kwani  kutokana na taarifa ya mpaka kufikia mwezi jana April 2021 imesajili kwa 0.6%.

“Uhamasishaji ufanyike kwa kushirikiana na maafisa maendeleo ya Jamii ambao Wana weredi katika kuraghibisha, kuhamasisha  na kufanya uchechemuzi kwa Jamii ili kuongeza usajili katika Halmashauri ya Bumbuli”,  amesisitiza Bi. Mgomapayo.

Hata hivyo amesema kuwa kuna malalamiko ya wananchi baadhi ya maeneo kuandikishwa lakini majina yao hayaonekani kwenye mfumo , hivyo amegiza mratibu wa ICHF kwa.kushirikiana na CHMT kuhakikisha wananchi wote waliosajiliwaqanonekana kwenye mfumo na kupata huduma stahiki.

Katika upande mwingine Bi. Mgomapayo  amesema CHMT wanapokwenda kwenye ufuatiliaji katika vituo watembelee katika Ofisi za  Serikali za Kata na  vijiji ili kupata taarifa ya Matumizi ya vyandarua ili kuhakikisha Matumizi sahihi ya vyandarua yanazingatiwa. 

Serikali unatumia pesa nyingi Sana kwa ajili ya kugharimia vyandarua vyenye dawa kwa ajili ya kugawia  wananchi. Kuna baadhi ya maeneo vyandarua vina tumika kwa kufugia vifaranga, kuvulia samaki na kufunikia bustani. Kama hakutakuwa na Matumizi sahihi ya vyandarua, lengo la Serikali la kutokomeza malaria ifikapo 2030 halitafikiwa.

Vile vile ametaka  uhamasishaji na elimu iendelee kutolewa kwa kushirikiana na maafisa maendeleo ya Jamii ili kubadilisha mitazamo hasi ya Jamii kuhusu Matumizi ya vyandarua  ili kuongeza Matumizi ya vyandarua na hatimae kutokomeza malaria.

 

Job Opportunity at ECODIT, Call for Experts: USAID Tanzania Marine Conservation Activity – Heshimu Bahari

WhatsApp Voice Messages Review Tool Being Tested for Android, iOS: Report