Katika taarifa, shirika la afya duniani limesema kwamba kiwango cha maambukizi ya virusi vya Corona hakijabadilika kwa muda wa siku saba kufikia Januari tarehe 9.

Afrika Kusini, ambako maambukizi mengi yameripotiwa Afrika, imeripoti kwamba maambukizi yamepungua kwa asilimia 14.

Shirika la Afya Duniani limesema kwamba maambukizi ya corona nchini Afrika kusini, ambapo virusi vya Omicron viligunduliwa, yamepungua kwa asilimia 9. Maambukizi pia yamepungua katika nchi za Afrika mashariki na kati.

Maambukizi hata hivyo yameongezeka katika nchi za Afrika kaskazini kwa asilimia 121.

Maambukizi pia yameongezeka Afrika Magharibi katika kipindi cha wiki moja iliyopita.

Dkt Abdou Salam Gueye, mkuu wa idara ya kusimamia majanga barani Afrika katika shirika la WHO amesema imechukua muda mfupi kwa Omicron kusambaa sana ikilinganishwa na Delta.

Dkt Gueye anaeleza: “Kufikia sasa, nchi 30 za Afrika zimegundua na kuripoti maambukizi ya Omicron. Katika nchi ambazo maambukizi yamesambaa sana, Omicron imegunduliwa sana na kwa haraka. Ilichukua muda wa wiki mbili kwa Delta kwa kulinganisha, ilichukua Delta wiki nne kufikia Beta katika viwango vya maambukizi

Tagged in: