By Sharon Sauwa

Dodoma. Watu tisa wamefariki dunia na wengine zaidi ya 30 wamejeruhiwa baada ya basi  la Emigrace linalofanya safari zake kati ya Babati Mkoa wa Manyara na Dar es Salaam kupinduka.

Ajali hiyo imetokea leo Jumamosi Oktoba 2, 2021  katika mteremko wa milima ya Kolo Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Besta Magoma amesema miili ya watu hao imehifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Kondoa.

“Bado tunaendelea na uokoaji,  idadi kamili ya majeruhi tutaijua baada ya kumaliza. Sasa hivi tunaendelea kuwapa rufaa majeruhi kwenda katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma,”amesema.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Onesmo Lyanga hakupatikana kulizungumzia tukio hilo.

This article Belongs to

News Source link

About the Author

Publisher

Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

View All Articles