AfricaSwahili News

Watu wawili wajaribu kumchoma kisu kiongozi wa mpito wa Mali Msikitini

Wanaume wawili wamejaribu kumdunga kisu rais wa mpito wa Mali Assimi Goïta katika msikiti uliopo katika mji mkuu, Bamako.

KanaliGoïta allikuwa akihudhuria ibada ya siku ya Eid ul-Adha katika msikiti wa Grand Mosque.

Mafisa wanasema washambuliaji, ambao kwa mujibu wa Shirika la habari la AFP walikuwa ni wawili, wamekamatwa na rais ameondolewa kwenye msikiti huo kwa usalama wake.

Haijafahamika iwapo Kanali Goïta, ambaye aliongozajeshi kuchukua mamlaka mwezi Agosti, alijeruhiwa.

Waziri wa masuala ya kidini Mamadou Kone aliliambia shirika la AFP kwamba mwanaume ali “jaribu kumuua rais wa kisu”.

Mkurugenzi wa msikiti aliliambia shirika la habari kwamba mtu alimlenga waziri lakini alimjeruhi mtu mwingine.

Kabla ya mapinduzi ya mwezi Agosti nchi hiyo ilikuwa inakabiliwa na maadamano juu ya ufisadi na waasi wa Kiislam walikuwa wameyateka maeneo mengi ya nchi.

Kanali Goïta aliingilia kati tena mwezi Mei, akachukua nafasi ya serikali ya mpito na kuchukua mamlaka kama rais- aliahidi kukabidhi utawala wa kiraia mamlaka kama ilivyopangwa mwaka ujao.

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.