More
  - Advertisement -

  Wawekezaji wacharuka waibukia mkoa wa Pwani, Wapania kujenga kiwanda cha simu za mkononi

  -

  - Ad Keep reading below -

  Victor Masangu, Pwani. 

  - Ad Keep reading below -

  SERIKALI ya Mkoa wa Pwani katika kuhakikisha inatekeleza kwa vitendo  azma ya kuwa na uchumi wa viwanda na kuwapa fursa wawekezaji  wa ndani na nje ya nchi imekutana na baadhi Wawakilishi (Delegation) kutoka Chemba ya Wafanyabiashara wa Kichina Tanzania (Chinese Business Chamber in Tanzania) kwa lengo la kujadili na kupanga mikakati ya kupata ardhi kwa ajili ya ujenzi wa viwanda.

  Katika kikao hicho ambacho kiliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani na kuhudhuliwa na baadhi ya viongozi mbali mbali wa Mkoa lengo ikiwa ni kufanya mazungumzo na wawakilishi hao kwa ambayo yataweza kuleta mabadiliko chanya  ya kimaendeleo kupitia sekta ya uwekezaji wa viwanda mbali mbali ambavyo vikikamilika vitaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi katika  kutoa fursa za ajira na kukuza uchumi.

  - Ad Keep reading below -

   Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo alibainisha kwamba lengo kubwa la ujio wa wawakilishi hao ni kuweza  kutafuta eneo la ardhi kwa ajili ya Ujenzi wa Viwanda ikiwa ni kutekeleza maombi waliyowasilisha kwa Mhe Rais walipokutana na kufanya mazungumzo Aprili, 21 mwaka  2021.

  ALSO READ  Ditopile aeleza mafanikio ya Serikali ya Dk. Magufuli kwenye sekta ya elimu
  ALSO READ  Kilimo bora cha Mchicha - MUUNGWANA BLOG

  “Tumepokea ugeni huu  na katika mazungumzo yao ujumbe huo umekuja kwa lengo kutafuta Ardhi kwa ajili ya Ujenzi wa Viwanda ikiwa ni kutekeleza maombi waliyowasilisha kwa Mhe Rais walipokutana na kufanya mazungumzo hivi karibuni kwa hiyo sisi kama Mkoa wa Pwani suala hili tutalifanyia kazi ili kuwapatia ardhi ya kujenga viwanda,”alisema Ndikilo.

  Aidha katika hatua nyingine  Ndikilo  amewatoa hofu kwa kuwahakikishia wawakilishi hao wa wafanyabiashara kuwa Mkoa  bado una maeneo ambayo tayari yametengwa  maalumu kwa ajili ya Ujenzi wa Viwanda hivyo watahakikisha wanawapa ushirikiano wa kutosha katika kila hatu ili waweze kutimiza malengo waliyojiwekea,

  Pia Ndikilo  amependekeza  kwa Wawekezaji hao kuwekeza  kwenye eneo la Kwala ambalo Jumla ya Hekta 500 wanazohitaji zitapatikana, na kuwaeleza kuwa  eneo la Kwala linafaa kwa Uwekezaji huo wa ujenzi wa Viwanda (Industrial Park).

  - Ad Keep reading below -

  Katika hatua nyingine alifafanua kuwa katika eneo la Kwala kwa sasa lina Miundombinu mbinu yote Muhimu ikiwemo, Maji ya uhakika, Barabara, Umeme wa uhakika ukaribu na Bandari kavu, ukaribu wa Reli ya Mwendokasi, na ukaribu na Jiji la Dar es salaam.

  ALSO READ  TAMISEMI Queens Mabingwa Wapya Ligi ya Muungano Zanzibar 2019
  ALSO READ  It will be cheaper for Nigeria to remain one country – Bishop Kukah

  Wawekezaji hao wakiongozwa na Bw. Janson Huang  wameeleza kuwa wanategemea kujenga na kuanzisha viwanda  zaidi ya 200 vya kuzalisha bidhaa mbali ikiwemo madawa, Kuunganishia pikiki, Viyoyozi, simu za mikononi  hivyo hitaji lao la kwanza ni Ardhi ila waendelee na michakato mingine ya Uwekezaji

   

  - read any article below now-
  Publisher
  Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

  Latest news

  Red Cross lacking partnership of Taraba Govt – Scribe

  The leadership of the Taraba State branch of the Nigeria Red Cross has lamented what it called the lukewarm attitudes of the state government...

  Filming of Disney sequel Disenchanted to begin in Irish locations on Monday

  Filming on the much anticipated sequel to the Disney hit Enchanted is to begin on Monday. Disenchanted, the live-action/animated musical romantic comedy is the follow-up...

  Iran coronavirus update: 14k news cases, 386 deaths

  TEHRAN, May 09 (MNA) – According to the Iranian Health Ministry, 14,141 new COVID-19 infections have been detected across the country in the past...
  - Advertisement -

  You might also likeRELATED
  Recommended to you

  - Advertisement -
  %d bloggers like this: