Vyombo vya Habari nchini Haiti vimeripoti leo kuwa ofisi ya mwendesha mashtaka wa nchi hiyo imependekeza kushtakiwa kwa waziri mkuu wa mpito Ariel Henry kuhusiana na mauaji ya rais Jovenel Moise yaliyotokea mnamo mwezi Julai. 

 
Taarifa hizo ni kulingana na barua iliyotumwa na ofisi ya mwendesha mashtaka kwenda kwa jaji anayehusika na kesi ya mauaji ya rais Moise ambayo imeorodhesha madai ya kuhusika kwa waziri mkuu Henry kwenye mkasa huo. 
 
Inaarifiwa kuwa serikali imetoa tangazo la kumfuta kazi mwendesha mashtaka mkuu wa serikali baada ya ofisi yake kutuma pia barua nyingine kwa mamlaka za uhamiaji ikimzuia waziri mkuu Henry kuondoka nchini humo. 
 
Hayo yanajiri baada ya vyombo vya habari kuripoti kuwa hivi karibuni waziri mkuu Henry aliitwa mbele ya waendesha mashtaka kutoa maelezo juu ya mawasiliano ya simu aliyoyafanya na moja ya washukiwa wa mauaji ya rais Moise usiku wa siku ya shambulizi.

 

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles