Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima leo 22 /09/2021 jijini Dodoma, amekabidhi magari saba kwa ajili ya ufuatiliaji wa shughuli za afya mazingira na usafi katika mikoa mbalimbali.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dk. Dorothy amesema kuwa Wizara ya Afya inatekeleza programu ya huduma endelevu za Maji na Usafi wa mazingira yenye lengo la uboreshaji na upatikanaji wa maji na huduma za Usafi wa mazingira vijijini.

Aidha ameongeza kuwa Program hiyo inatekelezwa kwenye mikoa 17 katika Halmashauri 86 nchini, mikoa iliyopokea magari hayo siku ya leo ni mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Simiyu Geita, Tabora, Katavi, Singida, Rukwa, Songwe, Iringa, Manyara, Ruvuma, Lindi na Mtwara.

“Wizara itaendelea kuwezesha Halmashauri na Mikoa kitatua changamoto za usafiri kwa kadri itavyopata rasilimali fedha kupitia program hii pamoja na kutenga fedha za kununua vyombo vya usafiri ambapo kwa mwaka huu wa fedha itanunua magari mengine 5 kwaajili ya Mikoa,” amesema Dk. Dorothy.
 

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles