Advertisement Scroll To Keep Reading
AfricaSwahili News

Waziri wa maji kuwa mgeni rasmi maadhimisho ya kumi kwa mwaka 2021 ya siku ya moto Mara

Advertisement Scroll To Keep Reading

Na Timothy Itembe Mara.

Advertisement Scroll To Keep Reading

WAZIRI wa maji Jumaa Awesso anatarajiwa kuwa mgeni rasimi Septemba,15,2021kwenye kilele cha maadhimisho ya kumi ya siku ya Mto  Mara yanayofanyika wilayani Tarime mkoani Mara.

Lengo la maadhimisho hayo ni kutoa msukumo mkubwa wa kuhifadhi Bonde la Mto Mara unaoanzia milima ya mau nchini Kenya na kuishia Ziwa Victoria upande wa Tanzania.

Jambo lingine la maadhimisho hayo ni pamoja na kuendelea kulitangaza na kulifuatilia tukio mhimu la kuhama kwa wanyama katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Masai Mara nchini Kenya.

Akiongea Afisa uhusiano Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria,Perepetua Masaga alisema kuwa mto Mara ni chanzo cha maji shirikishi kinachojumuisha nchi mbili za Tanzania na Kenya chanzo cha mto Mara kinaanzia katika chemchem za Enapuiyapui katika misitu iliyopo  katika milima ya mau nchini Kenya na kupitia katika hifadhi ya masai Mara nchini Kenya na hatimaye kuingia hifadhi ya Serengeti (SENAPA) nchini Tanzania ukubwa wa eneo la Bonde ni 13,325km2 na urefu wa mto nitaklibani 400km.

Afisa huyo aliongeza kuwa uwepo wa mto Mara huchangia rasilimali Maji kwenye Ziwa Victoria vile vile huchangia kuwepo kwa Hifadhi ya Serengeti ambayo ni tegemeo kubwa la Taifa na wananchi jirani na hifadhi kutokana na shuguli za utalii.

 

Naye mkuu wa wilaya Tarime,Michael Mntenjele alisema serikali ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania ilitangaza kuanza kusimamia Rasilimali za Maji kwa mfumo wa kihaidrojia ya mabonde mnamo mwaka 1981 mwaka 2000 Bodi ya maji Bonde la Ziwa Victoria ilianzishwa.   

“Sisi wote tunatambua umhimu wa maji kwa maisha yetu ya kila siku ya Binadamu na viumbe wengine tunasema maji ni uhai kwa kuwa binadamu na viumbe wanahitaji maji ili waishi maji ni rasilimali mhimu sana katika kukuza na kuimarisha uchumi wa Taifa katika uzalishaji mali maji yote ni mali ya Taifa na yanasimamiwa chini ya sheria ya usimamizi wa Rasilimali za maji namba 11 ya mwaka 2009 lengo la sheria hii kuratibu na kusimamia matumizi bora ya Maji na kuzuia uchafunzi wa vyanzo vya maji”alisema Mntenjele.

Mntenjele  alitumia nafasi hiyo kuitaka jamii kutunza kulinda na kudhibiti uchafuzi wa vyanzo vya maji kwa kuzingatia sheria iliyopo vinginevyo atakaye bainika akikaidi sheria hiyo na kufanya shuguli za kibinadamu ndani ya mita zilizokatazwa sheria itachukua mkondowake.

 

Advertisement Scroll To Keep Reading

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.