Advertisement Scroll To Keep Reading
AfricaSwahili News

Wito watolewa kutambua miili iliyotolewa kutoka mtoni, Kenya

Advertisement Scroll To Keep Reading

Kikundi cha kutetea haki za binadamu nchini Kenya kimehimiza serikali kusaidia kutambua miili 16 iliyoopolewa kutoka Mto Tana katika mkoa wa kaskazini mashariki katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

“Baadhi ya familia zinaweza kukosa rasilimali ya kuwasafirisha huko kwa zoezi la utambuzi wa mwili,” Hussein Khalid, mkurugenzi mtendaji wa Haki Africa, aliambia BBC.

Advertisement Scroll To Keep Reading

Alikuwa akijibu mwito wa polisi kwa wale wanaotafuta jamaa waliopotea kutembelea chumba cha kuhifadhi maiti katika kaunti ya Garissa.

Miili iliyopatikana imeoza sana, wengine walikuwa wamefungwa kamba mikononi na miguuni, wengine walikuwa wamefungwa mawe kwa kuzunguka, ripoti ya vyombo vya habari nchini humo zimesema.

Hakuna miili yoyote iliyokuwa na aina yoyote ya hati za kitambulisho juu yao.

Polisi wanasema waathiriwa waliuawa na miili yao kutupwa mtoni, kituo cha runinga ya eneo ya Citizen TV.

Familia zingine zinazotafuta jamaa wao waliopotea huku wakiwa na wasiwasi, walitembelea chumba cha kuhifadhia maiti huko Garissa Jumatatu lakini wakaondoka wakiwa wamevunjika moyo.

<

p data-reactid=”.1du2a3kn5du.2.0.0.1.0.1.0.$lx-tabs0.0.$lx-commentary.$lx-commentary.2.0.1.1.1:$post-6140bd28455e0f06d48a05d3.0.6.0.0:$post_9″>Sampuli kutoka kwa miili hiyo sasa imepelekwa katika maabara ya serikali kwa uchunguzi.

 

Advertisement Scroll To Keep Reading

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ? Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

Related Articles

Back to top button

AdBlock Detected

If you enjoy our content, Please support our site by disabling your adblocker. We depend on ad revenue to keep creating quality content for you to enjoy for free.