By Waandishi Wetu

BAADA ya kushindwa kutetea taji la Mapinduzi uongozi wa klabu ya Yanga umewapongeza watani zao Simba kwa kutwaa taji hilo huku ikitamba kupambana kupata yaliyobaki.

Simba ndio mabingwa wa Mapinduzi baada ya kuwafunga mabingwa mara nyingi wa taji hilo Azam FC bao 1-0.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha aliwapongeza Simba kwa kutwaa taji hilo huku akiweka wazi kuwa kwao sasa wamesahau mambo ya Mapinduzi wanaangalia Ligi.

“Nawapongeza watani kwa kutwaa taji, Yanga tumeshasahau kuhusu Mapinduzi tunamchezo wa ligi dhidi ya Coastol Union na mingine lengo ni kuhakikisha tunafanya vizuri huko,” alisema na kuongeza kuwa;

“Tumepoteza kombe moja la Mapinduzi tumeshapokea kosa hili sasa tunapambana kufanya vizuri kwenye ligi na mashindano mengine,” alisema.News Source link

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles