Serikali ya Rwanda imetangaza kwamba wanafunzi zaidi ya 60,000 watalazimika kurudia masomo baada ya kufanya vibaya kwenye mitihani yao.

Kati ya hao zaidi ya wanafunzi 44,000 walifanya mitihani ya kuhitimu shule ya msingi, na wengine waliobaki walifanya mitihani ya sekondari.

Mwaka jana Mamlaka za elimu nchini zilianzisha sera maaalumu ya kusaidia kuongeza ufaulu wa wanafunzi, kwa mujibu wa mtandao wa New Times.

Waziri wa elimu wa nchi hiyo alisema wanafunzi watakaokuwa na maswali watasaidiwa, kwa mujibu wa sera hiyo.

“Hatua inayofuata”, kwa mujibu wa Valentine Uwamariya ni “kufuatilia wanafunzi na shule zao, na baadaye kutakuwa na mpango maalumu wa kuwasaidia, kwa kushirkiana na bodi ya elimu ya Rwanda (REB), wilaya na shule”.

Uamuzi huo uliibua hasira hasa kwneye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya watu wakisema sio wa haki.

Waziri wa elimu alikubali kukosolewa huko na kusema serikali haitadharau ukweli kwamba baadhi ya watoto wanaweza kuacha shule kutokana na uamuzi huo, kwa mujibu wa The New Times.

“Tuna matumaini kwamba kwa sababu kuna mpango maalumu wa kuwasadia, hawawezi kuvunjika moyo ” alisema.

 

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles