HATABIRIKI
Siyo watu wakutabirika, ni watu wenye hisia za kubadilika badilika, mara muda huu ana furaha na kuonesha mapenzi, mara ghafla anakasirika na kutaka kuadhibu mtu.

MKATILI
Ni wenye tabia ya mabavu hususani katika tendo la ndoa, hawatajali hisia zako, umelala usingizini au unaumwa, bali hujali zaidi kuzitimiza haja zao.

LAWAMA
Huwa na tabia ya kuwalaumu sana wengine kwa matatizo anayo yapata, Mfano anapo kosa kazi, anapo-shindwa shuleni. Kila kitu ni kosa la mtu mwingine na siyo yeye.

WIVU
Mpenzi wako anakuwa na wivu sana kwa ule muda unaotumia kuwa na wafanyakazi wenzako, marafiki na hata ndugu zako, ingawa siyo kwamba anataka muda huo awe na wewe.

Tagged in:

About the Author

Dr john Masawe

Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?Founder, CEO, Admin and Publisher Of This Website

View All Articles